You are here

Press Release: Kagera Earthquake happened in Tanzania

Date: 
14 Sep 2016

PRESS RELEASE ON KAGERA EARTHQUAKE 

Peoples Health Movement Tanzania (PHM Tanzania) is uniting with stakeholders and Tanzanians concerns about the effects of the earthquake occurred in the region of the lake, especially the municipality of Bukoba on Saturday September 10, 2016 Afternoon.

 

However, PHM Tanzania offers congratulations to the government to address the issue of where the government was based rendering first aid to the victims of the earthquake.

 

PHM Tanzania underscores the government continues to manage social services such as sewage disposal and avert possible outbreaks of disease. Also many victims have been sleeping outside for fear of collapsing house for most of 1200 and more have found homes cracks.

 

PHM Tanzania has appealed to many stakeholders regardless of their position and their state support in the donation bank account provided by the State (Name of Account: Disaster Committee, account number: 0152225617300, Swiftcode: CORUtztz, CRDB Bank Bukoba). We hope our contribution will help access to health care as protective drugs, vaccines and mosquito net for many families, especially women and children who have been sleeping outside. The rainy season is approaching and so residents are afraid of the spread of malaria epidemics faster.

 

PHM Tanzania has appealed to the victims with the government actively manage sanitation and food in the camps set up in order to prevent epidemics and bring more potential impediments to the victims of the earthquake.

 

PHM Tanzania calls the government to send construction professional  (Engineers) to check on residents who find cracks and provide advice as these homes are vulnerable to their homes or they can use them for survival while awaiting aid rehabilitation which continue being collected from anywhere in the world

 

'’Here's a look, especially those containing cracks suspicious as there are houses need to be rebuilt or repaired otherwise it will bring more disaster to householders when the falls occurs’’ PHM Tanzania spokesperson, Godfrey Philimon has described it.

 

Also PHM Tanzania calls the government to make the renewal assessment for victims and families to discover the elderly, pregnant mothers and children under five years old to be priorities in aids as required by our health policy.

 

PHM Tanzania calls the government to use its instruments of security such as the Police and the Army to protect properties and equipment mainly in damaged homes so that they cannot be stolen by evil men. Much more, protect relief commodities rehabilitation and reconstruction that have been supported by good Samaritans.

 

PHM Tanzania and its partners believe that tragedies like these contribute to poor public health and eventually missing dereliction of fundamental rights as public health policies, programs and national strategies envisaged. Also recognizes it is a challenge for the government as well as the general public. However, PHM Tanzania believes that in cooperation between citizens, government and stakeholders we can resolve the concerns brought by this tragedy of the earthquake to residents of Bukoba and Kagera region in general.

 

For More information contact:

Godfrey Philimon
Country Coordinator
PHM Tanzania
Tel: +255 659 977752
Email:[email protected]
Website: www.phmovement.org
Twitter: @phmtanzania

 

 

 

 

 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

Shirika lisilo la Kiserikali linaloshughulikia  Haki za Afya kwa Jamii (Peoples Health Movement Tanzania– PHM Tanzania) linaungana na wadau na watanzania kusikitishwa na madhara ya tetemeko lililotokea katika kanda ya ziwa hususani manispaa ya Bukoba siku ya jumamosi tarehe 10 Septemba 2016 Alasiri.

 

Hata hivyo, PHM Tanzania inatoa pongezi kwa serikali kwa kushughulikia suala hilo ambapo serikali imesimamia utoaji wa huduma ya kwanza kwa wahanga wa tetemeko la ardhi.

 

PHM Tanzania inasisitiza serikali kuendelea  kusimamia huduma za kijamii kama vile maji taka kutosambaa na kuepusha kutokea kwa milipuko ya magonjwa. Pia wahanga wengi wamekuwa wakilala nje kwa kuhofia kuangukiwa na nyumba kwani zaidi ya nyumba 1200 na zaidi zimepata nyufa.

 

PHM Tanzania inawaomba wadau wengi bila kujali nafasi zao na hali zao kusaidia uchangiaji katika akaunti ya banki iliyotolewa na Serikali (Jina la Akaunti: Kamati ya Maafa, Akaunti namba: 0152225617300, Swiftcode: CORUtztz, CRDB Bank Bukoba). Ni matumaini yetu PHM Tanzania michango itasaidia upatikanaji wa huduma za afya kama madawa ya kinga, chanjo na net za mbu kwani familia nyingi hasa wanawake na watoto wamekuwa wakilala nje. Msimu wa mvua unakaribia na hivyo wakazi wana hofu ya kuenea kwa malaria na magonjwa ya milipuko kwa kasi.

 

PHM Tanzania inawaomba wahanga pamoja na serikali kusimamia kikamilifu usafi wa mazingira na vyakula katika kambi zilizoanzishwa ili kuzuia magonjwa ya milipuko yanayoweza kujitokeza na kuleta zaidi kero kwa wahanga wa tetemeko la ardhi.

 

PHM Tanzania inaiomba serikali kutuma wataalamu wa ujenzi (Engineers) kuwapitia wakazi waliopata nyufa na kutoa ushauri kama nyumba hizo ni hatarishi kwa makazi yao au wanaweza kuzitumia kwa ajili ya kuishi wakati wanasubiri misaada ya ukarabati unayoendelea kukusanywa kutoka sehemu mbali mbali nchini na dunia  

 

‘Hapa tuangalie hasa zile zenye nyufa za kutia mashaka kama kuna nyumba zinahitaji kujengwa upya au kurekebishwa bila hivyo kitakachofuatia majanga ya kudondokewa na nyumba,’ msemaji wa PHM Tanzania, Godfrey Philimon ameeleza hayo.

 

Pia PHM Tanzania inaiomba serikali kufanya tathimini upya kwa waathirika na kugundua familia zenye wazee, wamama wajawazito na watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ili wawe vipau mbele katika misaada inayochangishwa kama sera yetu ya afya inavyoelekeza.

 

PHM Tanzania tunaiomba serikali kwa kutumia vyombo vyake vya usalama kama polisi na jeshi kulinda mali na vifaa hasa katika nyumba zilizoharibiwa ili visiweze kuibiwa na watu wabaya. Na zaidi kulinda misaada ya mali ghafi za ukarabati na ujenzi watakazopelekewa.

 

PHM Tanzania na wadau wake wanaamini kuwa majanga kama haya yanachangia wananchi kukosa afya na hatimaye kutotekeleza haki za msingi za afya kwa jamii kama sera, mipango  na mikakati ya kitaifa inavyoelekeza. Pia inatambua ni changamoto kwa serikali pamoja na wananchi kwa ujumla. PHM Tanzania inaamini kwa ushirikiano kati ya wananchi, serikali na wadau mbali mbali tutaweza kutatua kero zilizoletwa na hili janga la tetemeko la ardhi kwa wakazi wa Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla.

 

Kwa maelezo Zaidi wasiliana na:

 

 

 

 

 

 

Godfrey Philimon

 

Mratibu Taifa

 

PHM Tanzania

 

Tel: +255 659 977752

 

Email:[email protected]

 

Website: www.phmovement.org

 

Twitter: @phmtanzania

 

 

 

 

 

PHM Circles: